Kenya Certificate of Primary Education
KCPE Past Papers 2021 Kiswahili Maswali
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Uhifadhi _l_ mito ni jambo _2__ lizingatiwe na wote. Wanajamii wengi __3_ taka mitoni bila __4_ hatari ya tendo lao. Ni lazima kama __5____ kuilinda mito. lnashangaza kuona 6 watu anavyoichafua wakisahau kuwa __7__. Uchafuzi huu ukiendelea __8_ tutajutia vitendo vyetu. Jamii inapaswa kuwajibika kwa kutupa _9_ la taka mahali panapofaa.
1. A. ya B. wa C. kwa D. mwa
2. A. linalofaa B. linayofaa C. linapofaa D. linakofaa
3. A. walitupa B. wakitupa C. wanatupa D.wangetupa
4. A. kuwazisha B. kuwazishwa C. kuwaziwa D. kuwazia
5. A. ibada B. mauti C. sheria D. desturi
6. A. kwamba B. jmsi C. kama D. Japo
7. A. ukupigao ndio ukufunzao. C. mchimba kisima huingia yeye mwenyewe. B. mwenye macho haambiwi tazama. D. ukiona vyaelea vimeundwa.
8. A. mp aka B. kisha c. angaa D. huenda
9. A. topa B. biwi C. bumba D. tuta
Kufanya kazi kwa bidii _10_ najamii _11_jadi. Kila mwanajamii alitarajiwa _12_kadiri ya nguvu _13_ilimradi akipate chakula. Kizazi cha sasa kinahitaji kuhamasishwa _14_mbinu bora za kilimo _15_zaraa.
10. A. kulijaribiwa B. kulithaminiwa C. kulichaguliwa D. kulisimamiwa
11. A. hata B. hadi C. toka D. tena
12. A. kujitolea mhanga B. kujitia ujuzi C. kujipa moyo D. kujitunua kifua
13. A. z.ake B. zao C. zetu D. zako
14. A. kati ya B. JUU ya c. licha ya D. zaidi ya
15. A. () B. C. D. /
Kutoka nambari 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.
16. Neno mwanasheria lina silabi ngapi?
A. 4 B. 5 c. 6 D. 7
17. Chagua kivumishi cha nomino katika sentensi ifuatayo: Mkulima msomi ameyahifadhi mazao tele kwenye ghala..
A. Yule.
B. Tele.
C. Msomi.
D. Kubwa.
18. kwa maneno ni:
A. humusi tano
B. thumuni tano
C. thumuni tatu
D. humusi tatu.
19. Chagua wingi wa sentensi: Mhandisi aliuondoa waya wa umeme uliokuwa ukining’inia kwake.
A. Wahandisi waliziondoa nyaya za umeme zilizokuwa zikining’inia kwake.
B. Wahandisi waliziondoa nyaya za umeme zilizokuwa zikining’mia kwao.
C. Wahandisi waliuondoa waya wa urneme uliokuwa ukining’inia kwao.
D. Wahandisi waliuondoa waya wa urneme uliokuwa ukining’inia kwake.
20. Kilemba ni ada wapewayo wajomba wa Bi. Harusi ilhali pesa za kuanzisha biashara huitwa:
A. ridhaa
B. bakshishi
C. mtaji
D. arbuni.
21. Chagua sentensi ambayo ina kiambishi ‘ni’ cha kuonyesha hali ya kuamuru.
A. Nendeni mkamsalimie babu.
B. Mtazuru Bonde la Ufa lini?
C. Alinisaidia kuvuka mto huo mpana.
D. Wakulima wanalima shambani.
22. Ipi si maana ya neno panda?
A. Kupuliza ala ya muziki.
B. Mahali ambapo njia zimegawika.
C. Enda kuelekea juu ya kitu.
D. Kifaa cha kutupiajiwe.
23. Chagua ukanusho wa: Kiranja alichaguliwa kwani alikuwa amehitimu.
A. Kiranja hajachaguliwa kwani hakuwa amehitimu.
B. Kiranja hakuchaguliwa kwani hakuwa amehitimu.
C. Kiranja hakuchaguliwa kwani hajakuwa amehitimu.
D. Kiranja hajachaguliwa kwani hajakuwa amehitimu.
24. Chagua udogo wa sentensi ifuatayo: Mshipi wa mtoto umewekwa ndani ya sanduku.
A. Kishipi cha mtoto kimewekwa ndani ya kisanduku.
B. Kishipi cha mtoto kimewekwa ndani ya sanduku.
C. Kisbipi cha kitoto kimewekwa ndani ya kisanduku.
D. Kishipi cha kitoto kimewekwa ndani ya sanduku.
25. Ngonjera ni shairi
A. lililo na vina vinavyobadilikabadilika katika kila ubeti
B. linalokaririwa na watu wawili au zaidi kwa kujibizana
C. lililo na mshororo wa mwisho ambao unaorudiwarudiwa
D. linalosimulia tukio fulani na buwa na kipande kimoja.
26. Chagua jibu lenye nomino iliyoundwa kutokana na kitenzi.
A. unda – muundo.
B. pungua – pungufu.
C. safisha – safi.
D. tii – mtiifu.
27. Chagua matumizi ya neno karlba katika sentensi ifuatayo: Tulipokea karibu shilingi milioni tatu kwa ujenzi wa bweni.
A. Kiasi.
B. Nusura.
C. Kutimia kwajambo.
D. Kuwa mbali kidogo,
28. Onyesha usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo: “Mtazuru mbuga ya wanyama kesho”. Mwalimu alisema
A. kuwa tutazuru mbuga ya wanyama siku hiyo
B. kuwa watazuru mbuga ya wanyama siku iliyofuata
C. kuwa wangezuru mbuga ya wanyama siku iliyofuata
D. tungezuru mbuga ya wanyama siku hiyo.
29. Ni sentensi ipi iliyo sahlhi kisarufi?
A. Mtoto mwenye anakimbia ametuzwa.
B. Mwalimu aliyenifunza ana maarifa mengi.
C. Kinyonga hicho kimepotelea kichakani mle.
D. Kule ndiko alimoingia fisi.
30. Rita na Fasi ni ndugu. Fasi atamwitaje mtoto wa Rita?
A. Mpwa.
B. Binamu.
C. Umbu.
D. Halati.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40
Bila shaka unazielewa hatua ambazo kila mja hupitia hadi kufikia utu uzima. Mojawapo ya hatua hizo ni ile ya kuwa mtoto. Nchini Kenya, yeyote ambaye hajafikisha umri wa miaka kumi na minane huchukuliwa kuwa mtoto. Ni muhimu kutaja kuwa mtoto awe wa jins ia ya kike au ya kiume ana haki ambazo kila mwanajamii anapaswa kuzifahamu.
Je, kiumbe huyu ana haki zipi ambazo zinahitaji kulindwa katika ulimwengu wa sasa? Haki za watoto zimekuwa zikipigiwa debe katika kitengo cha kitaifa na cha kimataifa. Kwa mfano, Umoja wa Mataifa una mkataba ambao unazibainisha haki za watoto; ambao umetiwa sahihi na mataifa wanachama. Kenya haijaachwa nje katika mkataba huo. Katiba yetu katika Sura ya nne, Kipengele cha 53 imetambua haki za mtoto kwa kina. K wa hakika, ni vyema tufahamu kuwa uhai wa mwanadamu huanza tu mama anapopata ujauzito. Kiumbe huyu anayebebwa ana haki ya kuishi. Ni hatia kwa mama mjamzito kuiavya mimba.
Vilevile mtoto anastahili kupewa jina pindi anapozaliwa iti kumtambulisha katika jamii yake. Fauka ya hayo, mtoto anahitaji malezi mema iii akue inavyostahili. Anapaswa kupata lishe bora itakayomwezesha kuwa na siha njema.
Lishe hii, itakuwa kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama vile kwashakoo na utapiamlo, Ni jukumu la mlezi kuhakikisha kuwa chakula alacho mtoto kina virutubishi vifaavyo kama vile wanga, protini, vitamini na madini yafaayo. Iwapo ataugua yampasa mlezi kumpeleka katika kituo cha afya ili lrupata matibabu yanayofaa. Isitoshe ni jukumu la mlezi kuhakikisha kuwa mtoto anaishi katika mazingira salama na safi.
Usalama anaoupata mtoto utamkinga dhidi ya hatari kama vile utekaji nyara, ubakaji, vitisho na pia hofu. Hali kadhalika, ipo haja ya mtoto kukingwa kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya anga kama vile baridi kali na joto jingi. Hali hizi hutokea hususan misimu ya masika, kipupwe, kiangazi na mapukutiko. Ni muhimu pia kuhakikisha kuwa mtoto anapewa chakula kilichotayarishwa kwa njia safi. Usafi wa malazi na mavazi nao usipuuzwe. Kadhalika mtoto akifikisha umri wa miaka minne anapaswa kupelekwa shuleni ili apate elimu ambayo ni ufunguo wa milango ya heri maishani.
Elimu hii itamwezesha kufanya maamuzi yafaayo. Hakika walioelimika wana mitazamo mipana kuhusu maisha, wakilinganishwa na wenzao ambao walikosa nafasi ya kupata elimu. Maarifa kutokana na elimu humwezesha mtoto kutangamana na wengine, kujieleza kwa urahisi na kuwa mbunifu. Baadhi yao wameweza kuchangia uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, kujipatia ajira na hata kubuni nafasi za kazi kwa wengine.
Ni wazi kuwa elimu ni hazina na akiba salama ambayo huwezi kupokonywa. Licha ya kuwa jamii kupitia Mashirika ya kutetea haki za watoto imejitolea kwa jino na ukucha kuzilinda haki hizo, juhudi hizi zimetingwa na changamoto si haba. Umaskini ni kikwazo kimojawapo kinachowafanya walezi kushindwa kuwatimizia watoto wao mahitaji ya kimsingi.
Si ajabu watoto katika baadhi ya familia kukosa hata kopo la uji asubuhi na hivyo kushinda njaa mchana kutwa. Wengine wao hawamudu kuwanunulia wanao mavazi ya kuwasetiri wala kuwapa mahali pa kuishi.
Yamkini watoto hawa wanapokosa mahitaji hayo hulazimika kuzimbua riziki kwa kushiriki ajira ya watoto. Utawapata watoto wakitumiwa na walanguzi katika biashara haramu ya dawa za kulevya, kufanyizwa kazi za sulubu kwa malipo duni na hata baadai yao kuwa windo jepesi katika ulanguzi wa watoto. Yakini, akosaye la mama hata la mbwa huamwa. Japo mila na desturi ni nguzo yajamii baadhi yazo huenda kinyume na haki za watoto. Kwa mfano, ndoa za mapema huathiri watoto kwani wanalazimika kuanzisha familia mapema hivyo hukosa nafasi ya kukua kama watoto.
Ukeketaji nao ni adui mkubwa kwa haki anazostahili msichana. Tendo hili humwathiri kiafya na kiakili. Inasikitisha kuona kwamba aliyepewa jukumu la kumkidhia mtoto mahitaji yake ndiye anayemdhulumu zaidi.
Kila mwanajamii anapaswa kuajibika iii kumtimizia haki zake. Mtoto naye aelekezwe kutambua na kutetea haki zake iii atimize ndoto zake maishani na kuwa mtu wa kutegemewa katika jamu.
31. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.
A. Kipindi muhimu zaidi ni kile cha kuwa mtoto.
B. Watoto wote wana nafasi ya kufikisha miaka kumi na minane.
C. Jamii ina wajibu wa kutambua maslahi ya watoto.
D. Binadamu wote w anazielewa haki za , atoto wa sasa na kuzilinda.
32. Ni jibu lipi sahihi kulingana na aya ya pill?
A. Hald za , atoto zimeangaziwa katika sehemu zote za ulimwengu.
B. Mataifa yote yameungana kujaclili kuhusu haki za mtoto.
C. Mataifa yote yamekubali kuzilinda haki za watoto wote.
D. Haki za watoto nchini Kenya zinahimizwa na mataifa mengine.
33. Chagua jibu lisilo sahihi kuhusu Katiba ya Kenya kulingana na kifungu.
A. Inatetea mahitaji ya mtoto kikamilifu.
B. Inathamini maisha ya mama mzazi.
C. Ina sheria zinazounga mkono makubaliano ya umoja wa mataifa,
D. Ina mwongozo kuhusu umuhimu wa maisha ya binaclamu.
34. Chagua jibu sahihi kuhusu mtoto kulingana na aya ya tatu.
A. Akiwa na jina husifika kote kijijini.
B. Akilelewa vizuri atakuwa mwenye nguvu.
C. Akila chakula cha kutosha afya huimarika.
D. Akidhoofika kiafya atafutiwe huduma ifaayo.
35. Ni jibu lipi lisiloonyesha jukumu la mlezi lrulingana na aya ya one?
A. Kumlinda mtoto kutokana na maovu yanayoweza kumkumba.
B. Kumtengea mtoto nafasi nzuri ya kulala katika chumba chake.
C. Kuhakikisha kuwa mtoto ana mavazi mwafaka vipindi mbalimbali.
D. Kuandaa chakula cha mtoto katika mazingira yanayofaa.
36. Kulingana na aya ya tano
A. mtoto asipopata elimu atatatizika maishani mwake
B. elimu inakuza mawazo ya waliosoma zaidi
C. elimu itamwezesha mtoto kujitegemea baada ya kuhitimu
D. mtoto asipopata elimu atashindwa kuhusiana na wengine.
37. Kwa mujibu wa kifungu, athari za umaskini kwa mtoto ni
A. kukosa chakula na kutumikishwa katika umri mdogo
B. kuwa na mavazi haba na makazi duni
C. kutumia dawa za kulevya na kuziuzia wenzao
D. kuwindwa na wanabiashara na kulipwa mshahara mdogo.
38. Chagua jibu linaloonyesha kuwa mtoto anadhulumiwa kwa mujibu wa aya ya saba.
A. Kuteswa kimawazo na watu anaowaamnn.
B. Kushirikishwa katika tamaduni zilizopitwa na wakati.
C. Kulazimishwa kuoa au kuolewa wakiwa wachanga. D. Kuaibishwa kupitia tendo la ukeketaji.
39. Maana ya ‘zimetingwa’ kulingana na kifungu ni?
A. Zimetengwa.
B. Zimetatizwa.
C. Zimekazwa.
D. Zimefungwa.
40. Kauli ‘elimu ni hazina’ imetumia tamathali gani ya usemi?
A. Tashbihi.
B. Nahau.
C. Sitiari.
D. Chu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Sungura alikuwa na mazoea ya kuamka alfajiri mbichi na kuelekea kwa marafiki zake hata kabla ya kunawa uso. Alidai kuwajulia hali japo alikuwa na sababu ambayo ilikuwa siri yake. . “Nani mwerevu kama mimi? Nala chakula chao kwa mpango!” Sungura alijichekea kila aliporejea kwake jioni huku tumbo lake limejaa ndi! Alijiona mwerevu sana akiamini kuwa akili ni nywele kila mtu ana zake.
Wanyama wengi hawakufurahishwa na tabia hiyo ya kuchukiza ya maenzao .kwani ilionyesha uzembe mtupu ambao ulipingwa sana. Wao walithamini wito wa kutendakazi wa bidii wakiami kuwa mgaagaa na upwa hali wali mkavu. Si kwamba Sungura hakuwa amefikiwa na malalamiko hayo lakini aliyatia masikio yake nta na kuamua kuendelea na hila zake.
Alizidi kufaidika kutokana na jasho la wenzake bila kujali. Alijiambia kimoyomoyo, “Kweli dunia haikosi mazumbukuku.” . Siku moja kama ilivyokuwa kawaida yake, Sungura aliazimia kuwatembelea angaa marafiki watatu. Kati yao alikuwa Nguchiro. Alitaka kufika kwake asubuhi na mapema kwa ajili ya kiamshakinywa; hakutaka kukawia hata kidogo.
Alimwelewa vyema rafiki yake Nguchiro. Kwa mazoea ya kuiwahi staftahi mapema. Angechelewa angepata Nguchiro ameufuta mlo wake fyu na kujifanya kwamba neno chakula alilisikia tu katika hadithi za paukwa pakawa! Haya basi, Sungura alivaa malapa harakaharaka na kufyatuka kama risasi kuelekea kwa Nguchiro. Alishika kijia kilichoelekea kwa Nguchiro.
Punde alikumbuka kwamba kijia hicho kilipitia kiamboni mwa mzee Kobe. Sungura hakutaka kabisa kukutana na huyo mzee. Alidai kwamba alikuwa amekashifiwa na mzee Kobe hapo awali kutokana na tabia ya kutegemea vya wengine. Sungura alikerwa na Kobe, “Kwa nini kila wakati nikikutana naye ananiambia nitulie nyumbani nifanye kazi ili nile jasho langu? Shida iko wapi nikila vya wenyewe? Nani amemzuia kutembea? Khaa! Mzee kimbelembele; sitaki kuuona uso wake!”Alijisemea kimoyomoyo huku ameukunja uso.
Ilimlazimu Sungura kubadilisha njia kupitia msituni ili kumkwepa mzee Kobe. Alienda mkikimkiki akifuata ujia wa kuelekea upande wa magharibi. Hakujali kutatizwa na umande na ukungu wa asubuhi hiyo kwani alijua fika alichokuwa anakilenga. Sungura alishangaa kuona vile miti mingi ilivyokuwa imekatwa. Alikumbuka usiku mmoja maneno ya Ndovu akilalamika kuhusu vitendo vya binadamu, “Jamani! Hawa wataangamiza kabisa mazingira yetu.
Uchu wao wa kukata miti unatia hofu. Juzi tu kulikuwa na miti sufufu. Lakini ona leo . . .. ” Mawazo yake yalikatizwa ghafla. Akasikia sauti hafifu na yenye maumivu makali ikimwita, “Sungura rafiki! Sungura rafiki! Njoo unisaidie! Ni: .. sa .. .i ….. .i . . . . ” Sungura alishtuka ghaya ya kustuka. liitambu kama sauti ya mfalme wa nyika.
Aliyatupa macho yake huku na kule akamona Simba aliyeangukiwa na gogo la mti. Alinyatianyatia na kufika ahpokuwa Simba. Simba alimsihi sana Sungura amnusuru. Sungura alisita kwa kuhofia maisha yake. Nafsi yake ilimwonya maadamu aliuelewa ukali wa Simba. Hata hivyo, Simba hakuchoka kumrai hata akamwahidi nusu ya milki yake. Sungura alishawishika na kuamua kulisukuma gogo lile kwa nguvu zake zote. Kwa mara ya kwanza gogo halikusonga mara ya pili na ya tatu sungura akachoka.
Baada ya majaribio kadhaa gogo lilisalimu amri Simba akapata afueni. Simba hakupoteza wakati alimeukia Sungura na kumkaba koo huku akicheka kicheko cha ushindi. ‘Nimekuwa hapa siku mbili bila kula chochote, Mungu aniletee chakula halafu nikiachilie wewe ni kitoeo changu leo simba alimwambia Sungura aliyekuwa analengwalengwa na machozi. Wema wa Sungura uligeuka kuwa bala beluwa. Kweli asante ya punda ni mateke. Sungura alimsihi sana Simba asimle lakini kilio chake kiliambulia patu Simba alikataa katakata kumhurumia. kwa uchungu mwingi, Sungura alijuta na kujilaumu kutomsikiliza mzee Kobe.
41. Kulingana na aya ya kwanza
A. Sungura aliwatembelea marafiki zake bila kujulikana
B. Sungura alipenda kuamka mapema iii kujitafutia riziki
C. wenzake walikuwa na mazoea kumwona Sungura kila asubuhi
D. wenzake walijua mipango ya Sungura ya kila siku.
42. Aya ya pili imebainisha kwamba
A. wenzake Sungura walikuwa na mazoea ya kujitegemea kwa chakula
B. wanyama hawakutaka kushirikiana na Sungura kazini mwao
C. ujanja wa Sungura uliendelea kwani wenzake walishindwa kumshauri
D. manung’uniko ya wenzake ya kila wakati yalikuwa yanamuudhi Sungura.
43. Ni jibu lipi lisilo sahihi kumhusu Nguchiro kwa mujibu wa aya ya tatu?
A. Anawafahamu baadhi ya marafiki wake vizuri.
B. Alifanya mambo yake mapema.
C. Alitembelewa na Sungura kila asubuhi.
D. Aliwanyima baadhi ya wanyama vitu vyake.
44. Kulingana na kifungu, Sungura ni
A. mwenye tamaa, jasiri
B. mwenye majivuno, mnafiki
C. mwenye dharau, katili
D. mwenye huruma, msahaulifu.
45. Sungura alimchukia mzee Kobe kwa sababu
A. alipenda kumuuliza Sungura maswali ya familia yake
B. aliufahamu udhaifu wa Sungura
C. alimwonea wivu Sungura kwa namna alivyotembea
D. alijigamba kutokana na hekima aliyokuwa nayo.
46. Aya ya tano imebainisha kuwa
A. ujia wa kupitia msituni uliwasumbua wapita njia wengi,
B. Simba alipata majeraha mabaya kutokana na ajali iliyomfika.
C. wanajamii hawakujali masilahi ya wanyama walioishi msituni.
D. Sungura alichukizwa na uharibifu wa misitu uliosababishwa na wenzake.
47. Sungura aliamua kumsaidia Simba kwa kuwa
A. alimhurumia Simba aliyekuwa na maumivu makali
B. aliamini ana nguvu nyingi za kumwokoa Simba
C. angepata zawadi kutokana na wema aliomtendea
D. alifurahishwa na maneno matamu ya Simba.
48. Ni jibu lipi halionyeshi maana ya methali ni nywele kila mtu ana zake’ katika kifungu?
A. Sungura alifahamu udhaifu wa wanyama wengine hivyo akawa anawadanganya.
B. Nguchiro aliamka asubuhi kukila chakula chake iii asimsaidie Sungura.
C. Simba alifanikiwa kupata msaada wa Sungura licha ya Sungura kumwogopa.
D. Mzee Kobe alimlazimisha Sungura kufanya kazi na wanyama wengine.
49. Kauli, ‘gogo lilisalimu amri’ imetumia tamathali gani ya usemi?
A. Tashihisi.
B. Chuku. C. Sitiari. D. Methali.
50. Kauli, ‘aliyatia masikio nta’ ina maana
A. alichukia aliyoambiwa
B. alikaidi aliyoambiwa
C. alibagua aliyoambiwa
D. alihuzunikia aliyoambiwa.
Uhifadhi _1_ mito ni jambo _2__ lizingatiwe na wote. Wanajamii wengi _3_ taka mitoni
bila _4_hatari ya tendo lao. Ni lazima kama _5_kuilinda mito. lnashangaza kuona _6_ watu
wanavyoichafua wakisahau kuwa _7_ Uchafuzi huu ukiendelea _8_ tutajutia vitendo vyetu.
Jami iinapaswa kuwajibika kwa kutupa _9_ la taka mahali panapofaa.
1. A. ya B. wa✔ C. kwa D. mwa
2. A. linalofaa✔ B. linayofaa C. linapofaa D. linakofaa
3. A. walitupa B. wakitupa C. wanatupa ✔D.wangetupa
4. A. kuwazisha B. kuwazishwa C. kuwaziwa D. kuwazia✔
5. A. ibada✔ B. mauti C. sheria D. desturi
6. A. kwamba B. jinsi✔ C. kama D. Japo
7. A. ukupigao ndio ukufunzao. C. mchimba kisima huingia yeye mwenyewe.✔ B. mwenye macho haambiwi tazama. D. ukiona vyaelea vimeundwa.
8. A. mpaka B. kisha c. angaa D. huenda✔
9. A. topa B. biwi✔ C. bumba D. tuta
Kufanya kazi kwa bidii _10_ najamii _11_jadi. Kila mwanajamii alitarajiwa _12_kadiri ya nguvu _13_ilimradi akipate chakula. Kizazi cha sasa kinahitaji kuhamasishwa _14_mbinu bora za kilimo _15_zaraa.
10. A. kulijaribiwa B. kulithaminiwa✔ C. kulichaguliwa D. kulisimamiwa
11. A. hata B. hadi C. toka✔ D. tena
12. A. kujitolea mhanga✔ B. kujitia ujuzi C. kujipa moyo D. kujitunua kifua
13. A. zake✔ B. zao C. zetu D. zako
14. A. kati ya B. Juu ya✔ C. licha ya D. zaidi ya
15. A. () B. C. D. /✔
Kutoka nambari 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.
16. Neno mwanasheria lina silabi ngapi?
A. 4 B.✔ 5 c. 6 D. 7
17. Chagua kivumishi cha nomino katika sentensi ifuatayo: Mkulima msomi ameyahifadhi mazao tele kwenye ghala.
A. Yule.
B. Tele.
C. Msomi.✔
D. Kubwa.
18. kwa maneno ni:
A. humusi tano
B. thumuni tano
C. thumuni tatu
D. humusi tatu.✔
19. Chagua wingi wa sentensi: Mhandisi aliuondoa waya wa umeme uliokuwa ukining’inia kwake.
A. Wahandisi waliziondoa nyaya za umeme zilizokuwa zikining’inia kwake.
B. Wahandisi waliziondoa nyaya za umeme zilizokuwa zikining’mia kwao.✔
C. Wahandisi waliuondoa waya wa urneme uliokuwa ukining’inia kwao.
D. Wahandisi waliuondoa waya wa urneme uliokuwa ukining’inia kwake.
20. Kilemba ni ada wapewayo wajomba wa Bi. Harusi ilhali pesa za kuanzisha biashara huitwa:
A. ridhaa
B. bakshishi
C. mtaji✔
D. arbuni.
21. Chagua sentensi ambayo ina kiambishi ‘ni’ cha kuonyesha hali ya kuamuru.
A. Nendeni mkamsalimie babu.✔
B. Mtazuru Bonde la Ufa lini?
C. Alinisaidia kuvuka mto huo mpana.
D. Wakulima wanalima shambani.
22. Ipi si maana ya neno panda?
A. Kupuliza ala ya muziki.✔
B. Mahali ambapo njia zimegawika.
C. Enda kuelekea juu ya kitu.
D. Kifaa cha kutupiajiwe.
23. Chagua ukanusho wa: Kiranja alichaguliwa kwani alikuwa amehitimu.
A. Kiranja hajachaguliwa kwani hakuwa amehitimu.
B. Kiranja hakuchaguliwa kwani hakuwa amehitimu.✔
C. Kiranja hakuchaguliwa kwani hajakuwa amehitimu.
D. Kiranja hajachaguliwa kwani hajakuwa amehitimu.
24. Chagua udogo wa sentensi ifuatayo: Mshipi wa mtoto umewekwa ndani ya sanduku.
A. Kishipi cha mtoto kimewekwa ndani ya kisanduku.
B. Kishipi cha mtoto kimewekwa ndani ya sanduku.
C. Kishipi cha kitoto kimewekwa ndani ya kisanduku.✔
D. Kishipi cha kitoto kimewekwa ndani ya sanduku.
25. Ngonjera ni shairi
A. lililo na vina vinavyobadilikabadilika katika kila ubeti
B. linalokaririwa na watu wawili au zaidi kwa kujibizana✔
C. lililo na mshororo wa mwisho ambao unaorudiwarudiwa
D. linalosimulia tukio fulani na buwa na kipande kimoja.
26. Chagua jibu lenye nomino iliyoundwa kutokana na kitenzi.
A. unda – muundo.✔
B. pungua – pungufu.
C. safisha – safi.
D. tii – mtiifu.
27. Chagua matumizi ya neno karlba katika sentensi ifuatayo: Tulipokea karibu shilingi milioni tatu kwa ujenzi wa bweni.
A. Kiasi.✔
B. Nusura.
C. Kutimia kwajambo.
D. Kuwa mbali kidogo,
28. Onyesha usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo: “Mtazuru mbuga ya wanyama kesho”. Mwalimu alisema
A. kuwa tutazuru mbuga ya wanyama siku hiyo
B. kuwa watazuru mbuga ya wanyama siku iliyofuata
C. kuwa wangezuru mbuga ya wanyama siku iliyofuata✔
D. tungezuru mbuga ya wanyama siku hiyo.
29. Ni sentensi ipi iliyo sahlhi kisarufi?
A. Mtoto mwenye anakimbia ametuzwa.
B. Mwalimu aliyenifunza ana maarifa mengi.✔
C. Kinyonga hicho kimepotelea kichakani mle.
D. Kule ndiko alimoingia fisi.
30. Rita na Fasi ni ndugu. Fasi atamwitaje mtoto wa Rita?
A. Mpwa.✔
B. Binamu.
C. Umbu.
D. Halati.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40
Bila shaka unazielewa hatua ambazo kila mja hupitia hadi kufikia utu uzima. Mojawapo ya hatua hizo ni ile ya kuwa mtoto.
Nchini Kenya, yeyote ambaye hajafikisha umri wa miaka kumi na minane huchukuliwa kuwa mtoto. Ni muhimu kutaja kuwa mtoto awe wa jins ia ya kike au ya kiume ana haki ambazo kila mwanajamii anapaswa kuzifahamu.
Je, kiumbe huyu ana haki zipi ambazo zinahitaji kulindwa katika ulimwengu wa sasa? Haki za watoto zimekuwa zikipigiwa debe katika kitengo cha kitaifa na cha kimataifa.
Kwa mfano, Umoja wa Mataifa una mkataba ambao unazibainisha haki za watoto; ambao umetiwa sahihi na mataifa wanachama. Kenya haijaachwa nje katika mkataba huo.
Katiba yetu katika Sura ya nne, Kipengele cha 53 imetambua haki za mtoto kwa kina. K wa hakika, ni vyema tufahamu kuwa uhai wa mwanadamu huanza tu mama anapopata ujauzito. Kiumbe huyu anayebebwa ana haki ya kuishi. Ni hatia kwa mama mjamzito kuiavya mimba.
Vilevile mtoto anastahili kupewa jina pindi anapozaliwa iti kumtambulisha katika jamii yake.
Fauka ya hayo, mtoto anahitaji malezi mema iii akue inavyostahili. Anapaswa kupata lishe bora itakayomwezesha kuwa na siha njema.
Lishe hii, itakuwa kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama vile kwashakoo na utapiamlo, Ni jukumu la mlezi kuhakikisha kuwa chakula alacho mtoto kina virutubishi vifaavyo kama vile wanga, protini, vitamini na madini yafaayo.
Iwapo ataugua yampasa mlezi kumpeleka katika kituo cha afya ili lrupata matibabu yanayofaa. Isitoshe ni jukumu la mlezi kuhakikisha kuwa mtoto anaishi katika mazingira salama na safi.
Usalama anaoupata mtoto utamkinga dhidi ya hatari kama vile utekaji nyara, ubakaji, vitisho na pia hofu. Hali kadhalika, ipo haja ya mtoto kukingwa kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya anga kama vile baridi kali na joto jingi.
Hali hizi hutokea hususan misimu ya masika, kipupwe, kiangazi na mapukutiko. Ni muhimu pia kuhakikisha kuwa mtoto anapewa chakula kilichotayarishwa kwa njia safi.
Usafi wa malazi na mavazi nao usipuuzwe. Kadhalika mtoto akifikisha umri wa miaka minne anapaswa kupelekwa shuleni ili apate elimu ambayo ni ufunguo wa milango ya heri maishani.
Elimu hii itamwezesha kufanya maamuzi yafaayo. Hakika walioelimika wana mitazamo mipana kuhusu maisha, wakilinganishwa na wenzao ambao walikosa nafasi ya kupata elimu.
Maarifa kutokana na elimu humwezesha mtoto kutangamana na wengine, kujieleza kwa urahisi na kuwa mbunifu.
Baadhi yao wameweza kuchangia uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, kujipatia ajira na hata kubuni nafasi za kazi kwa wengine.
Ni wazi kuwa elimu ni hazina na akiba salama ambayo huwezi kupokonywa.
Licha ya kuwa jamii kupitia Mashirika ya kutetea haki za watoto imejitolea kwa jino na ukucha kuzilinda haki hizo, juhudi hizi zimetingwa na changamoto si haba.
Umaskini ni kikwazo kimojawapo kinachowafanya walezi kushindwa kuwatimizia watoto wao mahitaji ya kimsingi.
Si ajabu watoto katika baadhi ya familia kukosa hata kopo la uji asubuhi na hivyo kushinda njaa mchana kutwa.
Wengine wao hawamudu kuwanunulia wanao mavazi ya kuwasetiri wala kuwapa mahali pa kuishi.
Yamkini watoto hawa wanapokosa mahitaji hayo hulazimika kuzimbua riziki kwa kushiriki ajira ya watoto.
Utawapata watoto wakitumiwa na walanguzi katika biashara haramu ya dawa za kulevya, kufanyizwa kazi za sulubu kwa malipo duni na hata baadai yao kuwa windo jepesi katika ulanguzi wa watoto. Yakini, akosaye la mama hata la mbwa huamwa.
Japo mila na desturi ni nguzo yajamii baadhi yazo huenda kinyume na haki za watoto.
Kwa mfano, ndoa za mapema huathiri watoto kwani wanalazimika kuanzisha familia mapema hivyo hukosa nafasi ya kukua kama watoto.
Ukeketaji nao ni adui mkubwa kwa haki anazostahili msichana.
Tendo hili humwathiri kiafya na kiakili. Inasikitisha kuona kwamba aliyepewa jukumu la kumkidhia mtoto mahitaji yake ndiye anayemdhulumu zaidi.
Kila mwanajamii anapaswa kuajibika iii kumtimizia haki zake.
Mtoto naye aelekezwe kutambua na kutetea haki zake ili atimize ndoto zake maishani na kuwa mtu wa kutegemewa katika jamu.
31. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.
A. Kipindi muhimu zaidi ni kile cha kuwa mtoto.
B. Watoto wote wana nafasi ya kufikisha miaka kumi na minane.
C. Jamii ina wajibu wa kutambua maslahi ya watoto.✔
D. Binadamu wote w anazielewa haki za , atoto wa sasa na kuzilinda.
32. Ni jibu lipi sahihi kulingana na aya ya pill?
A. Hald za , atoto zimeangaziwa katika sehemu zote za ulimwengu.
B. Mataifa yote yameungana kujaclili kuhusu haki za mtoto.
C. Mataifa yote yamekubali kuzilinda haki za watoto wote.✔
D. Haki za watoto nchini Kenya zinahimizwa na mataifa mengine.
33. Chagua jibu lisilo sahihi kuhusu Katiba ya Kenya kulingana na kifungu.
A. Inatetea mahitaji ya mtoto kikamilifu.
B. Inathamini maisha ya mama mzazi.✔
C. Ina sheria zinazounga mkono makubaliano ya umoja wa mataifa,
D. Ina mwongozo kuhusu umuhimu wa maisha ya binaclamu.
34. Chagua jibu sahihi kuhusu mtoto kulingana na aya ya tatu.
A. Akiwa na jina husifika kote kijijini.
B. Akilelewa vizuri atakuwa mwenye nguvu.
C. Akila chakula cha kutosha afya huimarika.
D. Akidhoofika kiafya atafutiwe huduma ifaayo.✔
35. Ni jibu lipi lisiloonyesha jukumu la mlezi lrulingana na aya ya one?
A. Kumlinda mtoto kutokana na maovu yanayoweza kumkumba.
B. Kumtengea mtoto nafasi nzuri ya kulala katika chumba chake.✔
C. Kuhakikisha kuwa mtoto ana mavazi mwafaka vipindi mbalimbali.
D. Kuandaa chakula cha mtoto katika mazingira yanayofaa.
36. Kulingana na aya ya tano
A. mtoto asipopata elimu atatatizika maishani mwake
B. elimu inakuza mawazo ya waliosoma zaidi
C. elimu itamwezesha mtoto kujitegemea baada ya kuhitimu✔
D. mtoto asipopata elimu atashindwa kuhusiana na wengine.
37. Kwa mujibu wa kifungu, athari za umaskini kwa mtoto ni
A. kukosa chakula na kutumikishwa katika umri mdogo✔
B. kuwa na mavazi haba na makazi duni
C. kutumia dawa za kulevya na kuziuzia wenzao
D. kuwindwa na wanabiashara na kulipwa mshahara mdogo.
38. Chagua jibu linaloonyesha kuwa mtoto anadhulumiwa kwa mujibu wa aya ya saba.
A. Kuteswa kimawazo na watu anaowaamnn.
B. Kushirikishwa katika tamaduni zilizopitwa na wakati.✔
C. Kulazimishwa kuoa au kuolewa wakiwa wachanga. D. Kuaibishwa kupitia tendo la ukeketaji.
39. Maana ya ‘zimetingwa’ kulingana na kifungu ni?
A. Zimetengwa.
B. Zimetatizwa.✔
C. Zimekazwa.
D. Zimefungwa.
40. Kauli ‘elimu ni hazina’ imetumia tamathali gani ya usemi?
A. Tashbihi.
B. Nahau.
C. Sitiari.✔
D. Chu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Sungura alikuwa na mazoea ya kuamka alfajiri mbichi na kuelekea kwa marafiki zake hata kabla ya kunawa uso. Alidai kuwajulia hali japo alikuwa na sababu ambayo ilikuwa siri yake. .
“Nani mwerevu kama mimi? Nala chakula chao kwa mpango!” Sungura alijichekea kila aliporejea kwake jioni huku tumbo lake limejaa ndi! Alijiona mwerevu sana akiamini kuwa akili ni nywele kila mtu ana zake.
Wanyama wengi hawakufurahishwa na tabia hiyo ya kuchukiza ya maenzao .kwani ilionyesha uzembe mtupu ambao ulipingwa sana.
Wao walithamini wito wa kutendakazi wa bidii wakiami kuwa mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
Si kwamba Sungura hakuwa amefikiwa na malalamiko hayo lakini aliyatia masikio yake nta na kuamua kuendelea na hila zake.
Alizidi kufaidika kutokana na jasho la wenzake bila kujali. Alijiambia kimoyomoyo, “Kweli dunia haikosi mazumbukuku.” .
Siku moja kama ilivyokuwa kawaida yake, Sungura aliazimia kuwatembelea angaa marafiki watatu. Kati yao alikuwa Nguchiro. Alitaka kufika kwake asubuhi na mapema kwa ajili ya kiamshakinywa; hakutaka kukawia hata kidogo.
Alimwelewa vyema rafiki yake Nguchiro. Kwa mazoea ya kuiwahi staftahi mapema.
Angechelewa angepata Nguchiro ameufuta mlo wake fyu na kujifanya kwamba neno chakula alilisikia tu katika hadithi za paukwa pakawa! Haya basi, Sungura alivaa malapa harakaharaka na kufyatuka kama risasi kuelekea kwa Nguchiro.
Alishika kijia kilichoelekea kwa Nguchiro.
Punde alikumbuka kwamba kijia hicho kilipitia kiamboni mwa mzee Kobe. Sungura hakutaka kabisa kukutana na huyo mzee.
Alidai kwamba alikuwa amekashifiwa na mzee Kobe hapo awali kutokana na tabia ya kutegemea vya wengine.
Sungura alikerwa na Kobe, “Kwa nini kila wakati nikikutana naye ananiambia nitulie nyumbani nifanye kazi ili nile jasho langu?
Shida iko wapi nikila vya wenyewe? Nani amemzuia kutembea? Khaa! Mzee kimbelembele; sitaki kuuona uso wake!”Alijisemea kimoyomoyo huku ameukunja uso.
Ilimlazimu Sungura kubadilisha njia kupitia msituni ili kumkwepa mzee Kobe. Alienda mkikimkiki akifuata ujia wa kuelekea upande wa magharibi. Hakujali kutatizwa na umande na ukungu wa asubuhi hiyo kwani alijua fika alichokuwa anakilenga.
Sungura alishangaa kuona vile miti mingi ilivyokuwa imekatwa. Alikumbuka usiku mmoja maneno ya Ndovu akilalamika kuhusu vitendo vya binadamu, “Jamani! Hawa wataangamiza kabisa mazingira yetu.
Uchu wao wa kukata miti unatia hofu. Juzi tu kulikuwa na miti sufufu. Lakini ona leo . . .. ” Mawazo yake yalikatizwa ghafla.
Akasikia sauti hafifu na yenye maumivu makali ikimwita, “Sungura rafiki! Sungura rafiki! Njoo unisaidie! Ni: .. sa .. .i ….. .i . . . . ” Sungura alishtuka ghaya ya kustuka. liitambu kama sauti ya mfalme wa nyika.
Aliyatupa macho yake huku na kule akamona Simba aliyeangukiwa na gogo la mti. Alinyatianyatia na kufika ahpokuwa Simba.
Simba alimsihi sana Sungura amnusuru. Sungura alisita kwa kuhofia maisha yake. Nafsi yake ilimwonya maadamu aliuelewa ukali wa Simba. Hata hivyo, Simba hakuchoka kumrai hata akamwahidi nusu ya milki yake.
Sungura alishawishika na kuamua kulisukuma gogo lile kwa nguvu zake zote. Kwa mara ya kwanza gogo halikusonga mara ya pili na ya tatu sungura akachoka.
Baada ya majaribio kadhaa gogo lilisalimu amri Simba akapata afueni.
Simba hakupoteza wakati alimeukia Sungura na kumkaba koo huku akicheka kicheko cha ushindi.
‘Nimekuwa hapa siku mbili bila kula chochote, Mungu aniletee chakula halafu nikiachilie wewe ni kitoeo changu leo simba alimwambia Sungura aliyekuwa analengwalengwa na machozi.
Wema wa Sungura uligeuka kuwa bala beluwa. Kweli asante ya punda ni mateke.
Sungura alimsihi sana Simba asimle lakini kilio chake kiliambulia patu
Simba alikataa katakata kumhurumia. kwa uchungu mwingi, Sungura alijuta na kujilaumu kutomsikiliza mzee Kobe.
41. Kulingana na aya ya kwanza
A. Sungura aliwatembelea marafiki zake bila kujulikana
B. Sungura alipenda kuamka mapema iii kujitafutia riziki✔
C. wenzake walikuwa na mazoea kumwona Sungura kila asubuhi
D. wenzake walijua mipango ya Sungura ya kila siku.
42. Aya ya pili imebainisha kwamba
A. wenzake Sungura walikuwa na mazoea ya kujitegemea kwa chakula✔
B. wanyama hawakutaka kushirikiana na Sungura kazini mwao
C. ujanja wa Sungura uliendelea kwani wenzake walishindwa kumshauri
D. manung’uniko ya wenzake ya kila wakati yalikuwa yanamuudhi Sungura.
43. Ni jibu lipi lisilo sahihi kumhusu Nguchiro kwa mujibu wa aya ya tatu?
A. Anawafahamu baadhi ya marafiki wake vizuri.✔
B. Alifanya mambo yake mapema.
C. Alitembelewa na Sungura kila asubuhi.
D. Aliwanyima baadhi ya wanyama vitu vyake.
44. Kulingana na kifungu, Sungura ni
A. mwenye tamaa, jasiri
B. mwenye majivuno, mnafiki
C. mwenye dharau, katili
D. mwenye huruma, msahaulifu. ✔
45. Sungura alimchukia mzee Kobe kwa sababu
A. alipenda kumuuliza Sungura maswali ya familia yake
B. aliufahamu udhaifu wa Sungura✔
C. alimwonea wivu Sungura kwa namna alivyotembea
D. alijigamba kutokana na hekima aliyokuwa nayo.
46. Aya ya tano imebainisha kuwa
A. ujia wa kupitia msituni uliwasumbua wapita njia wengi,
B. Simba alipata majeraha mabaya kutokana na ajali iliyomfika.
C. wanajamii hawakujali masilahi ya wanyama walioishi msituni.✔
D. Sungura alichukizwa na uharibifu wa misitu uliosababishwa na wenzake.
47. Sungura aliamua kumsaidia Simba kwa kuwa
A. alimhurumia Simba aliyekuwa na maumivu makali
B. aliamini ana nguvu nyingi za kumwokoa Simba
C. angepata zawadi kutokana na wema aliomtendea
D. alifurahishwa na maneno matamu ya Simba.✔
48. Ni jibu lipi halionyeshi maana ya methali ni nywele kila mtu ana zake’ katika kifungu?
A. Sungura alifahamu udhaifu wa wanyama wengine hivyo akawa anawadanganya.
B. Nguchiro aliamka asubuhi kukila chakula chake iii asimsaidie Sungura.
C. Simba alifanikiwa kupata msaada wa Sungura licha ya Sungura kumwogopa.
D. Mzee Kobe alimlazimisha Sungura kufanya kazi na wanyama wengine. ✔
49. Kauli, ‘gogo lilisalimu amri’ imetumia tamathali gani ya usemi?
A. Tashihisi.✔
B. Chuku.
C. Sitiari.
D. Methali.
50. Kauli, ‘aliyatia masikio nta’ ina maana
A. alichukia aliyoambiwa
B. alikaidi aliyoambiwa✔
C. alibagua aliyoambiwa
D. alihuzunikia aliyoambiwa.