Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili Karatasi ya 1 – Insha
Maagizo

Andika insha mbili. lnsha ya kwanza ni ya lazima.

Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.

Kila insha isipungue maneno 400.

Kila insha ina alama 20.

Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

✤ Insha ya Lazima

  1. Wewe ni katibu wa jopokazi ambalo limeteuliwa kuchunguza sababu za wanafunzi wa shule za upili kupuuza masomo ya kiufundi. Andika ripoti ya uchunguzi huo huku ukitoa mapendekezo.

✤ Chagua insha nyingine moja kati ya hizi tatu zilizobakia.

  1. Maktaba ya shule yenu haina magazeti. Andika makala kuonyesha umuhimu wa maktaba hiyo kuwa na magazeti.
  2. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:

✤ Mpanda ovyo hula ovyo.

  1. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo:

✤ Msongamano wa wanunuzi, wapitanjia na wasukuma mkokoteni katikati mwa wachuuzi wa kila aina ulinitanabahisha kuwa nimefika mji wa Tafaruku.

Karatasi Ya 1 Insha Mwongozo Wa Kusahihisha

  1. Hii ni ripoti

Yafuatayo yazingatiwe:-

a) Muundo

Sura ya ripoti idhihirike

i) Kichwa – kionyeshe kiini cha uchunguzi

ii) Utangulizi

Mtahiniwa ataje jopokazi: wanachama walioteuliwa, aliyeteua jopokazi
Hadidu za rejea (Masharti na mipaka ya utekelezaji wa kazi iliyopangiwa
jopokazi)

Sampuli lengwa – habari zilikokusanywa
Njia za ukusanyaji – hojaji, mahojiano, majadiliano kwenye vikundi
iii) Mwili – Hoja zijadiliwe humu; vichwa vidogo vitumiwe

Sababu/mapuuza/matokeo
Mapendekezo
Hitimisho
Kimalizio
b) Maudhui

Baadhi ya hoja ni:-

i) Msisitizo mkubwa kwenye masomo ya kiakademia

2

ii) Kutokuwa na vielelezo tosha vy watu waliofanikiwa kwa kufuatia masomo ya

aina hii

iii) Masomo haya kutohimizwa katika shule nyingi kwa sababu ya ukosefu wa

vifaa

iv) Ukosefu wa walimu waliohitimu katika taaluma hizi

v) Shinikizo kutoka kwa wazazi – wanafunzi wajishughulishe na masomo

mengine

vi) Mtazamo hasi kuwa baadhi ya masomo kama vile ufundi wa mabomba ni duni

vii)Hapajawa na mfumo bayana unaoonyesha hatua ambazo

mwanafunzi/mwanagenzi atapitia hadi pengine Chuo kikuu

viii) Mafunzo mengine ya kiufundi ni ghali

ix) Vyuo vichache vya kiufundi katika sehemu ya mashambani

x) Vyuo vingine vya kiufundi vimegeuzwa kuwa vyuo vikuu, hivyo wanafunzi

kutoona umuhimu wa vyuo vya kiufundi

xi) Badhi huenda wasimudu masomo ya kisayansi, hivyo kukata tama

xii)Masomo haya yanahitaji mtaji ndipo anayesomea apate ajira

xiii) Mtazomo potovu uwa masomo haya ni ya mapato ya chini

xiv) Walimu kuwavunja wanafunzi moyo

xv) Masomo haya hayana mvuto kwa wanafunzi

xvi) Masom haya huwafunga wanafunzi kukhusika wenyewe

xvii) Mtazamo hari wa kijinsia kitamaduni, kitikadi

xviii) Hoja zingine siko wazi

c) Mahiniwa atoe angaa pendekezo moja kwa mafano

i) Mtala usisitize masomo ya kiiufundi kuanzia ngazi za chini

ii) Vyuo vya Ualimu vihusishe ufundishaji wa masomo ya kiufundi

iii) Serikali iongezse ufadhili kwa masomo ya kiufundi

iv) Kuwe na mfumo bayana unaoonyesha taaluma ambayo mwanafunzi atasomea

akifuatia masomo ya kiufundi

  1. Makala yaonyeshe umuhimu wa magazeti

Sura ya Makala idhihirike

Badhi ya hoja ni:-

i) Kujuza kuhusu yanayojiri nchini/ulimwenguni

ii) Kupalilia usomaji wa mapana

iii) Kukuza ubunifu – mwanafunzi atajifunza mitindo mbalimbali ya uandishi

iv) Kufunzia/kujifunzia sajili ya magazeti

v) Baath hula an sofa yak kufunzia vipengele vya lugha

vi) Hukuza stadi za kuhariri

vii)Hupalilia uwazaji wa kina, kwa mfano kupitia kujaza mraba

3

viii) Kupalilia mazoea ya kusoma

ix) Kufanikisha somo la maktaba

x) Kupalilia mbinu za kitafiti/mazoea ya kudadisi

xi) Kuburudisha

xii)Kuimarisha masomo kupitia kwa maswali na majibu

  1. Hii ni insha ya methali

Kisha kidhihirishe maana ifuatayo

Mtu asipotia bidii katika jambo matokeo yake huwa hafifu

AU

Kiasi cha kufanikiwa katika jambo hutegemea matayarisho/mikakati ambayo inawekwa

Baadhi ya hali ambazo zinaweza kujitokeza ni:-

i) Mwanafunzi kutojitayarisha ipasavyo kwa ajili ya mtihani na hatimaye kupata

alama zisizoridhisha

ii) Wakulima wakose kujiandaa ipasavyo, mwishowe wapate mavuno haba

iii) Shirika likose kuweka mikakati ifaayo kuimarisha pato lake; lisipate faida,

mwishowe lifilisike

iv) Mlezi kutowaelekeza watoto ipasavyo, watoto kuinukia kuwa wasiotegemewa

v) Mwajiri kutojaribu kuimarisha uhusiano wake na waajiriwa wake, migogoro izidi,

uzalishaji mali uathirike vibaya

Tanbihi

  1. Vipengele vitatu vya kimuundo vijitokeze; utangulizi, mwili, hitimisho
  2. Kichwa cha makala kidhihirike
  3. Sharti insha idhihirishe juhudi hafifu/mikakati hafifu/ukosefu wa kujiandaa, na baadaye

hali/matokeo yasiyoridhisha

Hii ni insha ya kibunilizi

Mtahiniwa atunge kisa ambacho kinaoana na mwanzo huu

Usimulizi unaweza kubainisha hali zifuatazo

i. Msimulizi asimulie yaliyotokea baada ya kuwasili, labda hata anaibiwa

ii. Msimulizi aonyeshe alikoenda baada ya kuwasili, labda anapokelewa na mwenyeji

wake; kasha asimulie maisha yake huko kwa mwenyeji wake

iii. Anaweza kuwa anapitia hapa tu; pengine anatoka garini kupumzika kabla ya

kuendelea na safari yake. Baadaye anaendeleza usimulizi wake hadi panapoishia

safari

iv. Msimulizi anaweza kuanza kwa kauli hizi, kasha ataturudhisha nyuma kusimulia kisa

ambacho kinamleta hapa

v. Anawea pia kusimulia maisha ya watu wa mji hu